August 22, 2016

Msimu wa 2016/2017 umeanza kwa kasi tayari kuna mipango mingi juu ya kutwaa ubingwa, ambapo Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amejipanga kuhakikisha anatetea ubingwa wa timu yake hiyo licha ya kutambua kuwa kuna ushindani mkubwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Yanga inatarajiwa kufungua pazia la ligi kuu dhidi ya African Lyon Agosti 28 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar, baada ya kukamilisha ratiba yao ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na TP Mazembe katika hatua ya makundi.
    


Yanga haijachezea mechi ya ligi kuu katika msimu huu kutokana na majukumu yao ya kimataifa wakati upande wa pili wapinzani wao, Simba wameshaanza mbio vizuri kwa kuifunga Ndanda FC mabao 3-1.

Akizungumza na Championi Jumatatu kabla ya jana kuondoka kuelekea DR Congo, Pluijm alisema anakiandaa kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu na kudai kuwa moja ya malengo yake ni kuhakikisha anafanikiwa kutetea ubingwa msimu huu.

“Nakiandaa kikosi changu kwa ajili ya msimu mpya, japokuwa wachezaji wangu watakuwa wamechoka kutokana na kutopumzika tangu msimu ulipoisha lakini tunahitaji kufanya vizuri.

“Lengo letu ni kutetea ubingwa japokuwa najua kuna ushindani mkubwa na tunachohitaji ni kuona tunafanya vizuri,” alisema Pluijm.

Msimu uiopita Yanga ilifanikiwa kutwaa ubingwa huku Azam FC ikimaliza katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi, hivyo Yanga itakuwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha inatetea ubingwa wao.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV