August 23, 2016

Straika chipukizi wa Manchester United, Marcus Rashford amepigwa mkwara na kocha wa timu yake ya taifa ya England, Sam Allardyce kuwa anaweza kupoteza nafasi ya kumuita katika timu ya taifa ikiwa ataendelea kuwekwa nechi katimu klabu yake.

Allardyce amesema hayo wakati huu ambapo anajiandaa kutangaza kikosi ambacho kitacheza dhidi ya Slovakia, mapema mwezi ujao.


Rashford ambaye alionyesha uwezo wa juu msimu uliopita katika kikosi cha vijana kabla ya baadaye kufanya hivyo katika kikosi cha wakubwa cha Man United amekosa nafasi ya uhakika tangu msimu huu uanze chini ya Kocha Jose Mourinho ambaye amekuwa akimtumia zaidi Zlatan Ibrahimovic.

 
Zlatan


Allardyce amenukuliwa akisema: “Ugumu ni kuwa Rashford hachezi inanipa wakati mgumu kumchagua. Naweza kufanya uamuzi wa kumwambia akacheze katika timu ya vijana ya U-21 ili azoee mikiki ya kimataifa, hiyo itamsaidia kupata nafasi hati katika klabu yake nma kisha timu ya taifa.”



Kauli hiyo ni kama mwiba kwa chipukizi huyo kwa kuwa ili apate nafasi anatakiwa kufanya kazi ya ziada mbele ya mkongwe Zlatan ambaye tangu atue kikosini hapo ameonekana kuwa hatari katika kufunga.

Aidha, Allardyce amesema kuwa anaweza kumpa nafasi Joe Hart lakini naye anatakiwa kupambana kupata namba kikosini kwake Manchester City ambapo amekosa uhakika wa kucheza tangu timu hiyo iwe chini ya Kocha Pep Guardiola.

Allardyce

Rashford




RATIBA YA MECHI ZA ENGLAND
Septemba 4: Slovakia  vs  England   Kufuzu World Cup
Oktoba 8: England       vs Malta        Kufuzu World Cup
Oktoba 11: Slovenia     vs England    Kufuzu World Cup
Novemba 11: England  vs Scotland   Kufuzu World Cup
Novemba 15: England  vs Spain        Kirafiki

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic