September 23, 2016Kuumia kwa mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi kumewakera mashabiki wa Borussia Monchengladbach.

Borussia Monchengladbach itakutana na FC Barcelona katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Jumatano.

Mashabiki hao wangefurahia kumuona Messi, taarifa za kuumia kwake katika mechi dhidi ya Atletico Madrid na kwamba atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu, zimewakera.

Kupitia mitandao ya kijamii, ikiwemo Twitter wamemtakia kila la kheri na apone haraka.

Wengi imeonyesha kuwashangaza kwa kuwa mchezaji hatari wa timu pinzani, huombewa asiwepo au asicheze vizuri.


Lakini mashabiki hao wa Borussia Monchengladbach walichotaka ni kumuona Messi uwanjani. Sasa hawajafurahia na wameweka hisia zao wazi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV