September 23, 2016


Muigizaji wa Bongo Muvi, Steven Jacob ‘JB’ ambaye ni Simba ‘damu’, ametambia kikosi chake kuwa lazima safari hii kilipize kisasi cha kufungwa na Yanga msimu uliopita, huku akidai Yanga ikijitahidi itafungwa walau kuanzia bao mbili kwenda juu.

JB, nyota wa filamu ya Shikamoo Mzee, alifunguka sababu zinazompa jeuri kuwa ni pacha kali ya Ibrahim Ajib, Laudit Mavugo na Shiza Kichuya ambayo imekuwa tishio tangu kuanza kwa msimu huu, akisisitiza kuwa bado hajaona safu ya ulinzi yenye kuwazuia.

“Hata wao wanalijua hilo kuwa hata siku moja Yanga haijawahi kucheza soka la kueleweka mbele ya Simba, ni bahati tu iliwaangukia maana ni msimu uliopita walifanya hivyo, siku nyingine walikuwa wakiogelea wao.

“Kwa aina ya kikosi na ari ya wachezaji kwa sasa, sioni Yanga wanawezaje kutufunga. Kasi ya washambuliaji Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo sijaona beki wa Yanga wa kuweza kuwazuia,” alitamba JB.


Aidha, JB alisema kuwa amepanga kuonana na wachezaji wa Simba kutoa ahadi yake kuelekea mchezo huo ili kuwaongezea motisha wapate ushindi katika mchezo huo utakaochezwa wiki ijayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV