October 1, 2016

AJIB (KULIA...
Straika wa Simba, Ibrahim Ajibu, amesema amejiandaa vizuri kucheza mechi ya leo dhidi ya Yanga na yupo tayari kupambana na beki yeyote iwe Vincent Bossou au Kelvin Yondani.

Ajibu, mwenye mabao mawili katika Ligi Kuu Bara, ameenda mbali kwa kusema beki yeyote atakayepangwa kati ya Bossou au Yondani, atahakikisha anakuwa uchochoro na kuitengenezea Simba mabao.

Ajibu alisema lengo lao ni kuona wanafanikiwa kushinda kila mechi katika mzunguko huu, hivyo haoni sababu ya kupoteza mechi ya leo.

“Timu yetu ipo vizuri na tunachohitaji ni kuona tunafunga katika kila mechi iliyo mbele yetu ikiwemo hii dhidi ya Yanga, tukipata pointi tatu kwa Yanga mambo yatakuwa mazuri.

“Najua kwenye mechi ya Yanga kutakuwa na upinzani mkubwa, hivyo nimejipanga vilivyo kukabiliana na beki yeyote atakayepangwa kunizuia, namuomba Mungu nisiumie hadi mwisho wa mchezo.


“Tunachokihitaji ni kuhakikisha tunafanikiwa kuibuka na pointi tatu katika mchezo huu halafu tuwafunge tena katika mzunguko wa pili wa ligi,” alisema Ajibu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV