October 1, 2016


Mara ya tatu? Haiwezekani. Hiyo ni kauli ya nahodha wa Simba, Jonas Mkude, akisema hawapo tayari kufungwa mara ya tatu mfululizo na Yanga wakati timu hizo zinapokutana leo.

Yanga na Simba leo zinacheza mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku kukiwa na kumbukumbu ya Simba kufungwa na Yanga mechi mbili zilizopita.

Mkude ambaye amekuwa nguzo muhimu kwenye kiungo cha Simba, alisema mchezo wa leo ni muhimu zaidi kwao na wana lengo la kushinda.

“Haitapendeza kuona tunapoteza mechi hii dhidi ya Yanga kutokana na mambo mawili yaliyopo mbele yetu, kwanza tunataka ubingwa, hivyo tumekubaliana kushinda kila mechi ikiwemo hii na Yanga.

“Pili, hatuwezi kukubali kufungwa mechi ya tatu mfululizo na Yanga kwani msimu uliopita wametufunga mechi zote mbili, hii inatuumiza na tumepanga kufuta vipigo hivyo,” alisema Mkude.

“Tumefanya maandalizi ya kutosha, tutaingia uwanjani tukiwa na ari ya kupambana kutokana na matokeo ya mechi zetu za nyuma na tuna morali ya kuwa kileleni, hivyo hatutaki kupoteza mechi.”


“Hakuna namna, lazima tushinde mchezo huu ili kufikia malengo tuliyojiwekea, kama tukifungwa itakuwa aibu kwetu kufungwa na Yanga mechi tatu mfululizo,” alisema Mkude.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV