October 2, 2016


Mitandao yote inayohusika na uonyeshaji mechi kwa kuandika LiveScore iliandika kwamba timu ya taifa ya vijana, Serengeti Boys imefuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika itakayofanyika nchini Madagascar, kesho.


Lakini baadaye kukawa na taarifa kwamba Serengeti Boys imeng’olewa baada ya kufungwa bao katika dakika ya 90+2.

Lakini baadaye tuliwapata viongozi wa TFF, Katibu Mkuu, MWesigwa Selestine amethibitisha Serengeti Boys imefungwa kwa bao hilo 1-0.

"Mtuwie radhi, hata sisi mwanzo tuliambiwa matokeo ni bila bila, hata mitandao yote kweli ilionyesha bilabila. Lakini mwisho tumepewa taarifa ambazo ni za uhakika kwamba tumefungwa kwa bao moja, dakika nne za nyongeza," alisema Mwesigwa.

1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV