October 1, 2016


Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Luis Suarez ameingia matatami tena baada ya kukumbana na tuhuma za kumtukana mwamuzi msaidizi.

Suarez anatuhumiwa kumtukukana mwamuzi huyo wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakicheza dhidi ya Borussia Monchengladbach ya Ujerumani na kupata ushindi wa mabao 2-1 wakiwa ugenini Ujerumani.

Mruguay huyo inaonekana akizungumza kwa jazba wakati akipinga uamuzi wa mwamuzi huyo na inaonekana alitukana au kutumia lugha chafu.

Bado haijathibitika na ikiwa hivyo, basi Suarez atakumbana na adhabu huku kukiwa na kumbukumbu ya matukio kadhaa aliyowahi kufanya yakiwemo yale ya kuwauma mabeki.

Kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es Salaam tayari kwa kazi ya kuwania pointi tatu dhidi ya watani wao Simba.

Yanga walikuwa kambini mjini Pemba kujiandaa na mechi hiyo ya leo dhidi ya Simba.

Simba waliokuwa Morogoro ndiyo walikuwa wa kwanza kufika jijini Dar es Salaam na wakafanikiwa kufanya mazoezi ya mwisho asubuhi.


Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu na presha imezidi kuwa juu zaidi huku kila upande ukionkena kujiamini kwamba una nafasi ya kushinda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV