January 26, 2017



Mjadala wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele kuachia ngazi katika klabu hiyo umeshika kasi.

Mjadala huo umekuwa na nafasi kubwa hasa mitandaoni, mashabiki wengi wa Simba wakihoji sababu ya kuachia ngazi siku chache kabla ya kuivaa Azam FC naye akiwa amerejea kuungana na Azam TV.

Kahemele aliwahi kufanya kazi Azam FC, baadaye Azam TV kabla ya kujiunga na Simba. Hii inaonyesha mashabiki hao wamekuwa na hofu kwa kuwa Simba inakutana na Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara, Jumamosi.

Jambo hilo limesababisha mashabiki katika makundi mbalimbali hasa yale ya Whatsapp na pia Facebook kuhoji, wengine wakidai huenda Kahemele alikuwa mtego kwao.

Lakini wako ambao wamekuwa wakiwatuliza wenzao na kuwataka kuwa na subira huku wakiamini Kahemele ni mtu ambaye pia anatakiwa kuangalia maslahi ambayo huenda yamemvuta.

Mara ya mwisho zilipokutana, Simba ililala kwa bao 1-0 dhidi ya Azam FC katika fainali ya Kombe la Mapinduzi, hiyo inaweza ikawa hofu namba moja ya Simba.

Lakini, inaonekana Simba wana hofu kwa kuwa wana tofauti ya pointi mbili tu dhidi ya Yanga, wao wana 45 na watani wao 43. Kama watapoteza na Yanga ikaishinda Mwadui, Jumapili. Basi watapoteza uongozi wa ligi kuu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic