January 28, 2017


 Serena Williams alimshinda dada yake Venus Williams na kubeba taji la Australian Open.

Ushindi huo dhidi ya Venus ambaye ni dada yake inakuwa ni Grand Slam ya  23 kwake.

Serena alishinda kwa seti mvili moja kwa moja yaani 6-4, 6-4 lakini kivutio zaidi ni dada hao walivyokuwa baada ya mechi.

Kumbuka makombe ya bingwa na mshindi wa pili yanakwenda kwenye familia moja.

Wawili hao walioanza tenisi kocha akiwa baba yao mzazi, walionekana ni wenye furaha, waliokuwa wakitaniana na hakuna aliyeonekana kuwa na masikitiko au furaha zaidi ya mwenzake.Baada ya fainali, mambo yalivyokuwa ni kama hakukuwa na chochote kilichopita na kila mmoja alionekana ameridhika kabisa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV