Mashabiki wa Yanga, wametamba kwamba wao hawana sababu ya kushangilia kwa nguvu kwa kuwa kuifunga Simba ni jambo la kawaida kabisa.
Kundi la wanachama na mashabiki katika tawi la Ubungo Teminal jijini Dar es Salaam, wametamba kwamba wamekuwa wakifanya mambo yao kwa utaratibu kwa kuwa kuifunga Simba, si jambo geni kwao.
“Kuna sababu gani ya kushangilia kwa juhudi kubwa, hawa wenzetu ni watu wa kelele. Hawana kawaida ya kutushinda, mara nyingi wanaanza na kushangilia na wanaishia kwenye kulaumiana.
“Sisi tumezoea kushinda dhidi yao, hakuna haja ya kelele nyingi. Tunawakimbiza kimyakimya tu, Jumamosi utaona,” alisema Mohammed Seif huku akishangiliwa na wenzake.
Mashabiki hao wametamba kwamba wana uhakika wa kushinda mechi hiyo na wameandaa aina mpya ya ushangiliaji kwa madai hakuna tawi lenye uwezo mkubwa wa kushangilia kama tawi lao.
0 COMMENTS:
Post a Comment