February 22, 2017





Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye (Mb) kesho Februari 23, 2017 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa miguu kwa vijana na wanawake.

Uzinduzi huo utakaofanyika saa 5.00 asubuhi, utahudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Mkurugenzi wa Michezo, Yussuph Singo. Utafanyika kwenye Ukumbi wa 
Hoteli ya Courtyard, Upanga jijini Dar es Salaam.

Mfuko huo uko chini ya Mwenyekiti Bw. Tido Mhando ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Azam Media wakati Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo ni Bw. Dereck Murusuri.

Wajumbe wake ni Bi. Beatrice Singano, Bw. Ephraim Mafuru, Bw. Tarimba Abbas, Bw. Joseph Kahama, Bw. Salum Rupia na Bw. Meshack Bandawe.

Majukumu ya Kamati ya Mfuko huo ni kukusanya rasilimali kwa ajili ya kuendeshea program za TFF za maendeleo ya mpira wa vijana wa wanawake.

Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, mfuko huu ni huru, una sekretariet yake, akaunti yake benki na ofisi zake zinazotarajiwa kuwa Mikocheni, Dar es Salaam.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic