March 27, 2017



Kikosi cha Azam FC kinachojiandaa kupambana na Yanga Jumamosi ijayo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, kimeingiwa na hofu juu ya mchezo huo baada ya kocha wake msaidizi, Idd Nassor Cheche kusema katika maandalizi yao kuna vitu wanavikosa.

Aprili Mosi, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar, Yanga na Azam zinatarajiwa kupambana kuelekea michezo ya mwisho ya kuhitimisha msimu huu ambapo mara ya mwisho timu hizo kukutana kwenye ligi zilitoka suluhu.

Azam ambayo inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 44, imekuwa ikijiandaa kupambana na Yanga huku ikiwakosa nyota wake saba waliopo katika kikosi cha Taifa Stars ambao ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Frank Domayo, Salum Abubakar na Himid Mao.

Cheche amesema: “Siku zote maandalizi ya pamoja ndiyo mazuri lakini inapotokea wachezaji wengi wamekosekana lazima kunakuwa na athari.

“Kwa sasa tunatafuta namna ya kufanya ili kukabiliana na hali hiyo kwa sababu ukiachana na siku hizi chache ambazo wengine hawapo, hapo nyuma walikuwa pamoja, hivyo kilichobaki tuombe Mungu huko walipo wasipate majeraha ili siku ya mchezo wetu dhidi ya Yanga wawepo wote.


“Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu, lakini tunaamini kadiri siku zinavyokwenda tutajua uwezo wetu wa kupambana nao umefikia wapi ila kwa sasa tunafahamu kwamba mchezo utakuwa mgumu kutokana na kwamba kuna timu zinasaka ubingwa na nyingine zikitafuta kulinda heshima.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic