March 19, 2017
Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi anatarajia kufunga ndoa na mzazi mwenzake na mpenzi wake wa siku nyingi, Antonella Roccuzzo lakini  rafiki yake, Gerard Pique hajaalikwa.

Pique hajaalikwa katika shughuli hiyo kwa kuwa mke wake, Shakira ambaye ni mwanamuziki haelewani na Antonella.

Gazeti maarufu la Hispania la El Pais limeeleza, hali hiyo imesababisha 


Imeelezwa Antonella alikuwa rafiki mkubwa wa mpenzi wa zamani wa Pique aitwaye Nuria Tomas. Hivyo hakufurahishwa shoga yake kupokonywa ‘koloni’ na Shakira, hivyo amekuwa hana mahusiano naye mazuri.Kilichomkera Shakira ni kuona Antonella akiendelea kuwa na uhusiano wa karibu na Nuria na kuona kama alikuwa analitiwa.

Kutokana na hali hiyo, wawili hao kila mtu amekuwa na lake na Messi na Pique wamekuwa wakitembeleana lakini kila mmoja anapokwenda kwa mwenzake, basi hawezi kuwa na mkewe.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV