March 29, 2017Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime, ameibuka na kusema kuwa wamejipanga kikamilifu kukatisha mbio za ubingwa wa Simba kwa  kufanikiwa kuibuka na pointi tatu katika mchezo wao wa Jumatatu.

Kagera Sugar inatarajia kukutana na Simba Aprili tatu katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba kwenye mchezo ambao unatarajia kuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na historia ya timu hizo pindi zinapokutana.

Kagera Sugar ipo nafasi ya nne ya msimamo wa ligi ikiwa na pointi 42 nyuma ya Azam FC yenye pointi 44, huku Simba ikiongoza msimamo kwa kuwa na pointi 55 ikiwa inawania kutwaa ubingwa msimu huu.

Akizungumza na Championi Jumatano, Maxime amesema kuwa, kikosi chake kipo vizuri kuelekea katika mchezo huo na kudai kuwa hawatakubali kupoteza pointi tatu kwa Simba na badala yake anajipanga kuona wanakatisha mbio za ubingwa  wa Simba.

“Tunajiandaa vyema kuelekea mechi yetu dhidi ya Simba, kikosi chetu kipo vizuri na hatuna sababu ya kuwahofia kwa kuwa sisi tupo vizuri hata kama na wao hawajafungwa katika mechi za hivi karibuni na sisi pia hatujapoteza mechi za hivi karibuni.

“Tunahitaji kuona tunakatisha mbio za ubingwa wa Simba, tumejipanga kuweza kushinda mechi zetu zote zilizo mbele yetu ili kuweza kufanikiwa kumaliza katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi,” alisema Maxime.


1 COMMENTS:

  1. Bro kwanini usiwe unafanya review ya ulichoandika! ! ! ? Maana jina uliloandika ni la maximo akati unaongelea mexime

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV