April 10, 2017



Uongozi wa Simba umesema unajipanga kwa kuongeza nguvu katika mechi zake mbili za Kanda ya Ziwa dhidi ya Mbao FC na Toto ili waweze kuibuka na pointi sita muhimu.

Simba ambayo ilikuwa ikiongoza msimamo wa ligi kuu, imepoteza mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar wikiendi iliyopita na kujikuta katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 55 nyuma ya Yanga yenye pointi 56.

Leo Simba itavaana na Mbao FC katika moja ya michezo miwili ya ugenini waliyobakiza, mwingine ukiwa ni dhidi ya Toto Africans Aprili 15.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, alisema  kutokana na kupoteza mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar wanahitaji kupambana ikiwa ni pamoja na kuongeza nguvu katika mechi zao mbili zilizobakia Kanda ya Ziwa ili kuweza kushinda zote.

“Tunahitaji kupambana kuhakikisha tunashinda mechi zetu zote mbili zilizobakia kwa kuongeza nguvu katika michezo hiyo.


“Bado tunayo nafasi ya kuweza kutwaa ubingwa kwa kuwa bado kuna mechi tano na lolote linaweza kutokea kwani kikosi chetu kipo vizuri,” alisema Hans Poppe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic