April 9, 2017
Baada ya Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania au Kamati ya Saa 72, kufanya kikako chake, imetaka Yanga ipewe onyo baada ya mashabiki wake kumwaga maji vyumbani.


Mechi namba 195 (Yanga 1 vs Azam 0). Yanga haikuingia kwenye chumba chake cha kubadilishia nguo, kutokana na kuwa na maji yaliyomwagwa na wanachama wa klabu hiyo (makomandoo) muda mfupi kabla ya timu hiyo kuwasili uwanjani.Kamati imeelekeza klabu ya Yanga iandikiwe barua ya onyo, na kuitaka kuhakikisha wanachama wake wanaacha mara moja mtindo wa kumwaga maji vyumbani baada ya kuwa vimeshafanyiwa usafi na wafanyakazi wa uwanja tayari kwa ajili ya matumizi ya timu yao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV