April 9, 2017
Majimaji imetakiwa kusimamia masuala ya usalama ya timu wageni zinazopokwenda kucheza mkoani humo, la sivyo Uwanja wa Majimaji mjini Songea, utafungwa kutumika katika Ligi Kuu Bara.

Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania au Kamati ya Saa 72, ilifanya kikao chake juzi Ijumaa Aprili 7, 2017 jijini Dar es Salaam na kufikia uamuzi ufuatao. 


Mechi namba 200 (Majimaji 4 vs Toto Africans 1). Katika mechi hiyo, timu ya Toto Africans ilifanyiwa vurugu ikiwa njiani kurejea hotelini baada ya mechi hiyo ambapo viongozi wake wawili waliumizwa. Tukio hilo liliripotiwa Kituo cha Polisi, na kesi tayari iko kortini.


Kituo cha Songea (Uwanja wa Majimaji) kiandikiwe barua ya kuhakikisha hazitokei vurugu uwanjani hapo baada ya mechi ikiwemo kuhakikisha timu ngeni inatoka uwanjani salama hadi kwenye hoteli ilikofikia. Iwapo vurugu zitaendelea, Bodi ya Ligi itasimamisha matumizi ya kituo hicho kama ilivyoainishwa katika Kanuni ya 9(2) ya Ligi Kuu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV