May 20, 2017Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima ameamua kumpa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara mchezaji mwenzake wa timu hiyo, Simon Msuva huku yeye akijiweka pembeni.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) hivi karibuni lilitoa orodha ya wachezaji watano wanaowania tuzo hiyo ya mchezaji bora wakiwemo Niyonzima na Msuva, wengine ni Shiza Kichuya na Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ na Aishi Manula wa Azam FC.

Niyonzima raia wa Rwanda amesema kuwa; “Kiukweli Msuva ndiye anayestahili tuzo ya mchezaji bora wa ligi msimu huu, amefanya mambo mengi makubwa kwa klabu hadi hapa tulipo.

“Amefunga mabao mengi (14) ambayo yamekuwa msaada kwa timu pia ni mtu muhimu katika kutengeneza ushindi wetu katika mechi tunazocheza, Msuva ana mchango mkubwa Yanga.”

Niyonzima alisema anaamini hata yeye ametoa mchango katika timu lakini Msuva amefanya mambo mengi ya mafanikio ya Yanga msimu huu ndiyo maana anapaswa kuwa mchezaji bora.

“Siyo siri katika mechi ambazo Msuva hakucheza tumekuwa tukipambana sana kupata ushindi, sasa mtu kama huyu ndiye anayetakiwa kuwa mchezaji bora,” alisema Niyonzima.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV