June 4, 2017


Kikosi cha Nakuru All Stars kinashiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Kenya leo kimefanya mazoezi ikiwa ni sehemu ya kujiweka fiti kabla ya mechi yake ya Jumanne dhidi ya Simba.

Nakuru All Stars itacheza mechi yake ya kwanza ya michuano ya SportsPesa Super Cup dhidi ya Simba, Jumanne.

Wachezaji wa Nakuru All Stars walionekana ni wenye furaha ambao wamepania kuonyesha maajabu siku hiyo wakiamini wataimaliza Simba na kutinga nusu fainali ya SportsPesa Super Cup.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV