June 4, 2017


Hatimaye mshambulizi Paul Kiongera amerejea tena nchini, safari hii akiwa na timu yake ya AFC Leopards kwa ajili ya kushiriki michuano ya SportsPesa Super Cup.

Bingwa wa SportsPesa Super Cup atapata nafasi ya kucheza na Everton FC ya England.
Kiongera aliyewahi kuichezea Simba lakini mambo yakaenda kombo yuko nchini tayari kwa ajili ya michuano hiyo na leo alifanya mazoezi pamoja na wenzake wa kikosi cha AFC Leopards.

Leopards watakuwa dimbani kesho kuwavaa Singida United katika mechi ya siku ya kwanza ya michuano hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV