July 14, 2017Kama unakumbuka tulikueleza kuhusiana na safari ya kiungo Ramadhani Singano maarufu kama Messi kwenda kujiunga na na klabu ya Difaa Al Jadida ya nchini Morocco.

Singano ameonekana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), tayari kwa safari ya kwenda Morocco.

Singano anakwenda kujiunga na Difaa Al Jadida ambayo tayari imesaini mkataba wake wa awali na atarejea nyumbani Tanzania Januari, mwakani kwa mapumziko.

SALEHJEMBE ilikuwa ya kwanza kukueleza, Singano aligoma kusaini mkataba wa Azam FC.

SALEHJEMBE ikawa ya kwanza kukueleza Singano ameanza mazungumzo na klabu hiyo ya Morocco na sasa inakuwa ya kwanza kukueleza kwamba walishamalizana.


Msimu uliopita, Al Jajida ilishika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Morocco maarufu kama Botola nyuma ya mabingwa, Raja Casablanca. Maana yake itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV