Cristiano
Ronaldo anaendelea kuwa mfalme wa Real Madrid bila ya kujali kuna ugeni wa
Gareth Bale ambaye ni mchezaji ghali zaidi duniani katika uhamisho baada ya
pauni milioni 86 kutolewa.
Katika mkataba
wake mpya alioingia na Madrid, Ronaldo analipwa karibia mara mbili ya anachopata
Bale.
Katika mkataba
wake huo mpya anaingiza pauni milioni 15 kwa msimu baada ya kodi lakini kabla
ya kupata bonsai yake ya wiki na Bale anaingiza pauni milioni 8.3 kwa msimu.
Wawili
hao tayari wameonyesha makali yao katika mechi ya kwanza tu ya La Liga baada ya
kila mmoja kufunga bao moja wakati Madrid ilipotoka sare ya mabao 2-2 na
Villareal.










0 COMMENTS:
Post a Comment