August 7, 2017Kipa Mcameroon wa Yanga, Rostand Youthe, juzi Jumamosi amekataa kuvaa kitambaa cha unahodha.

Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi Jumamosi katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati timu hiyo ilipocheza dhidi ya Singida United.

Kipa huyo, mwenye umbile kubwa alijiunga na Yanga kwa kusaini mkataba wa miaka miwili hivi karibuni akitokea African Lyon ambayo imeshuka daraja.

Ishu nzima ilikuwa katika kipindi cha pili cha mchezo huo dakika ya 76 baada ya Kocha Mkuu wa Yanga Mzambia, George Lwandamina alifanya mabadiliko kwa kumtoa beki Kelvin Yondani na nafasi yake kuchukuliwa na Vincent Andrew 'Dante'.

Yondani awali alivaa kitambaa hicho cha unahodha kutoka kwa beki Nadir Haroub 'Cannavaro' aliyetolewa kipindi cha pili cha mchezo huo.

Wakati Yondani anatoka, akamfuata Mcameroon huyo na kumpatia kitambaa hicho ambacho alikikataa huku akimkwepa na baadaye Thabani Kamusoko akakifuata, akachukua na kukivaa.


Katika mechi hiyo, Yanga ilipata ushindi wa mabao 3-2,  mabao yao yakifungwa na Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe na Emmanuel Martin huku ya Singida yakipachikwa na Danny Usengimana na Simbarashe Nhiri.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV