August 4, 2017SIMBA SPORTS CLUB
DAR ES SALAAM
 3-8-2017

                
            TAARIFA KWA UMMA
       ___________

Klabu ya Simba inayo furaha kubwa ya kuanza mchakato wa elimu ya mabadiliko ya muundo wa klabu. 

Muundo huo unatokana na mabadiliko ya katiba yaliyofanywa na wanachama na kusajiliwa na msajili wa vilabu nchini. 

Kamati inayoratibu zoezi hilo itaanza kazi hiyo ya utoaji elimu jumamosi hii, kwa kukutana na Wenyeviti wa matawi, kwenye Semina itakayofanyika Makao makuu ya klabu, mtaa Msimbazi kuanzia saa tatu na nusu. 

Semina hiyo ya tarehe tano , itatanguliwa na nyingine zitakazofanyika kwenye wilaya zote za mkoani Dar es salaam, zikuhusisha wanachama wote kutoka kwenye wilaya hizo. 

Pamoja na semina hizo, kamati hiyo pia itatoa elimu kupitia Televisheni,vituo vya Redio na Magazeti,lengo likiwa kila mwanachama wa Simba awe na ufahamu mpana kabla ya mkutano maalum wa katiba wa tarehe ishirini ya mwezi ujao. 

Ratiba kamili ya semina nyingine tutaitoa mwishoni mwa wiki hii. 

IMETOLEWA NA... 

HAJI MANARA

MKUU WA HABARI SIMBA SC


SIMBA NGUVU MOJA

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV