September 23, 2017



Wakati kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, wenyeji Ruvu Shooting wametamba kuisimamisha Mtibwa Sugar isipate ushindi katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara.

Hadi sasa katika ligi hiyo, Mtibwa ipo kileleni ikiwa na pointi tisa katika mechi tatu ilizocheza na kushinda zote ambapo Ofisa Habari wa Ruvu, Masau Bwire amesema watawazima wapinzani wao kesho.

Bwire amesema wanajua kuwa mchezo huo utakuwa mgumu lakini wao wana uwezo wa kuwafunga Mtibwa na kuwastopisha mbio zao za kuwania ubingwa.

“Najua Mtibwa ni timu kubwa na ina uwezo, mchezo utakuwa mgumu lakini niwaambie tu sisi tuna uwezo wa kuwafunga Jumapili (kesho) kwenye uwanja wetu wa nyumbani kwani vijana wamejianda vizuri.

“Siku zote kumfunga mtu ambaye hajawahi kupoteza mechi hata moja ni jambo la furaha sana na sisi tunataka kuleta matumaini kwa mashabiki wetu kuwa bado Ruvu Shooting tuna uwezo,” alisema Bwire.

Wakati Mtibwa ikiwa nafasi ya kwanza, Ruvu yenyewe ipo nafasi ya 13 katika msimamo wa timu 16 za ligi kuu ikiwa na pointi mbili tu katika mechi tatu za ligi kwani imetoka sare mbili na kufugwa mara moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic