October 29, 2017




Na George Mganga
Kuingia kwa Simba uwanjani huku wakijiamini kuwa mechi itakuwa rahisi, sambamba na mashabiki kwenda na matokeo mfukoni siku ya jana, ndicho kilichopelekea hali kuwa tofauti.

Simba walicheza kwa kujiamini zaidi haswa kipindi cha kwanza huku Yanga wakipambana zaidi kusaka mabao.

Uimara wa safu ya kiungo iliyotumiwa vizuri na Kabamba 'mutu ya Congo' ilitengeza mipenyezo mingi kuwafikia washambuliaji wa mwisho.

Kuanza kwa James Kotei hakukuleta #Approach nzuri ya mchezo upande wa Simba, ingawa kwa mimi nilidhani Omog angemuanzisha Mkude ambaye ana uzoefu zaidi na hizi mechi. Alionesha mabadiliko baada ya kuingia kipindi cha pili.

Kingine Simba walibweteka ni kujiamini wana kikosi ghari kuliko Yanga, ilihali matokeo hayaamuliwi na gharama bali mandalizi.

Hii ni sawa na kipindi kile Yanga wanafungwa na Simba bao 3-1 katika mechi ya Mtani Jembe wakati huo Yanga wakiwa na nyota wengi na kikosi chao kikiwa na thamani kubwa kuliko Simba. Tukumbuke.

Moja ya nyota kutoka Yanga wakati huo alikuwa na Emmanuel Okwi ambaye alitumiwa pia kwenye mechi hiyo, kutambulishwa kwa mashabiki wa Yanga.

Ni sahihi kwa mashabiki wa Yanga kujinasibu na hiyo sare ya 1-1 kwa maana fikra nyingi kwa wengi walidhania mechi itakuwa ngumu zaidi kwao huku wa Simba wakijiamini.


Mwisho wa siku mpira ni dakika 90.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic