November 5, 2017



Nanodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ameumia goti na huenda akashindwa kurejea nchini Taifa Stars itakapocheza mechi ya kimataifa wiki ijayo.


Samatta ameumia goti wakati timu yake ya KRC Genk ilipoivaa Lokeren katika mechi ya Ligi Kuu ya Ubelgiji na kulazimika kupumzishwa katika dakika ya 40 ya mchezo.


Hata hivyo, Samatta atafanyiwa vipimo rasmi kesho ili kujua ameumia kiasi gani.

Kutoka Ubelgiji, Samatta ameithibitishia SALEHJEMBE kwamba ameumia na anasubiri vipimo.

"Ni kweli nimeumia, nasubiri suala la vipimo kesho ndiyo nitajua zaidi," alisema Samatta ambaye sasa ni tegemeo katika safu ya ushambulizi ya Genk.

Genk walilazimika kufanya mabadiliko na kumuingiza Nikos Karelis kuchukua nafasi ya Samatta aliyeumia. Mechi hiyo ambayo Genk walikuwa nyumbani iliisha kwa sare ya 0-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic