November 5, 2017



MPIRA UMEKWISHAAAA

Dk 90+3 Ndemla anageuka na kuachia mkwaju mkali hapa, goal kick
KADI Dk 90+3 Manula analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda


DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90 Kipa Fikirini analazimika kutoka nje ya eneo lake na kuokoa mpira kuwa wa kurusha
SUB Dk 88 Mohammed Ibrahim anaingia upande wa Simba kuchukua nafasi ya Kichuya
Dk 86 Simba wanaonekana kulinda zaidi huku wengi wakiwa wamerudi nyuma kuhakikisha wanalinda bao lao moja
SUB 82 Victor Hanganya anaingia kuchukua nafasi ya Mkopi upande Mbeya City
Dk 82 Mavugo anachanganya baiskeli na kuachia shuti kali, juuu
Dk 81 Mavugo katika nafasi nzuri kabisa, anapiga shuti mtoto
Dk 79 Manula analazimika kutoa mpira na kuwa kona, mpira unachongwa vizuri lakini Simba wanaokoa
SUB Dk 78 anaingia Mavugo na nafasi yake inachukuliwa na Laudit Mavugo
KADI Dk 77 Mohamed Mkopi analambwa kadi ya njano kwa ubabe dhidi ya Kotei


Dk 75 Okwi anawachambua mabeki wawili wa Mbeya City, yeye na kipa anaisha juuu
Dk 73 Simba wanaingia vizuri tena lakini Lundenga anaokoa unakua wa kurusha
Dk 73, Simba wanapoteza nafasi nzuri kabisa, Ndemla akiwa amebaki yeye na kipa lakini anampa mikononi
Dk 70 Simba inapata kona baada ya Lundenga kuutoa mpira akimdhibiti Okwi
KADI Dk 69 Okwi analambwa kadi ya njano kwa kumsukuma beki Mbeya City
Dk 68 sasa, Mbeya City wanaonekana kubadili mfumo wa ushambulizi na sasa zaidi wanapiga krosi ndefu
SUB Dk 64 Omari Ramadhani anakwenda nje baada ya kuumia anaingia Iddi Selemani Nado upande wa Mbeya City Dk 61 mchezaji mmoja wa Mbeya City anatolewa nje baada ya kubanwa na misuli
Dk 57, Lundenga anaachia mkwaju mkali wa mpira wa adhabu lakini unagonga ukuta wa Mbeya City


SUB Dk 55 Simba wanafanya mabadiliko ya kwanza, Niyonzima anakwenda benchi jirani na Omog na nafasi yake inachukuliwa na Said Hamisi Ndemla
Dk 54 Mkopi anaachia mkwaju mkali kabisa nje ya 18, Manula anadaka vizuri kabisa
Dk 51,Kotei analazimika kufanya kazi ya ziada dhidi ya Ambokile
Dk 49 Ambokile anajaribu kwa mara nyingine, anaachia shuti lakini goal kick
DK 47, Ambukile anaingia vizuri mbele ya Juuko lakini Zimbwe Jr anaokoa vizuri
KADI Dk 46 Ngassa analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Niyonzima
Dk 45 Kipindi cha pili kimeanza, taratibu mpira unafika katika lango la Mbeya City na Niyonzima anawekwa chini

MAPUMZIKO

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 45, Mbeya City wanaonekana kuendelea kikokaaa kutaka ksuawazisha
Dk 43 Muzamiru anachonga faulo safi, Nyoni na kipa, lakini kipa anaokoa vizuri kabisa
Dk 42 Niyonzima anawekwa chini, nje kidogo ya eneo la 18
Dk 40 sasa, bado inaonekana hakuna mashambulizi makali san ndani ya kila eneo la 18
Dk 35 Mbeya City wanarudisha mpira kwa kipa, ni hatari hapa lakini kipa anawahi na kuokoa
Dk 34 Ngassa anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, Manula anadaka unamtoka lakini anauwahi
Dk 32, mabeki City wanalazimika kufanya kazi ya ziada kumthibiti Kichuya

Dk 29 Kichuya anatoa pasi nzuri sana lakini Okwi anachelewa na mwamuzi anasema ni offside
Dk 25, Bocco anaingia vizuri kabisa lakini Kyaruzi anaokoa vizuri kabisa
Dk 22 mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja
Dk 17, Juuko analazimika kuokoa mpira wa kurushwa wa Mwasapili na kama angechelewa basi inekuwa shida
Dk 14 sasa, Mbeya City wanaonekana kuamka na kushambulia mfululizo wakiongozwa na Mrisho Ngassa lakini mipira yao mingi langoni mwa Simba imekuwa haina macho
Dk 10, Simba wanaingia vizuri tena, Bocco katika nafasi nzuri lakini anapoteza timing. Simba nao wanalalamika kuwa Bocco aliangushwa ndani ya 18


Dk 8, Mbeya City wanajibu mashambulizi hapa ndani ya eneo la hatari lango la Simba lakini Juuko anaosha hapa. Wachezaji City wanalalamika kuna mchezaji wa Simba ameshika pale
GOOOOOOOOOOOOOOO Dk 7 Kichuya anaipatia bao baada ya mpira mrefu kutoka katika ya uwanja kwa Mkude, mabeki wa Mbeya City kama wakazembe hivi
Dk 5, SImba wanaingia tena katika lango la City lakini umakini wakati wa kutupia krosi langoni unakuwa si mzuri
Dk 3, Simba wanafanya shambulizi kali, kipa Mbeya City analazimika kutoka nje kuokoa, lango halina mtu lakini Kichuya anabutua juuuu
Dk 1 mpira unaanza kwa kasi na krosi nzuri ndani ya lango la Simba, anaikosa hapa Babu Ally

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic