January 31, 2018




Kufuatia kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, benchi la Ufundi la Yanga, limetoa tathimini yake ya mechi za mzunguko huo na kukiri kuwa kwenye nafasi ya tatu.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo, wamemaliza mzunguko wa kwanza katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 28, nyuma ya Azam wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 30 wakati vinara wa ligi hiyo, Simba wakiongoza kwa pointi 35.

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa alisema kuwa kwa upande wao wanaamini hawakustahili kuwa katika nafasi hiyo na walipaswa kufanya vizuri zaidi ya hapo.

“Nadhani kwa upande wetu tulitakiwa tufanye vizuri zaidi ya hapa  tulipo sasa lakini  msimu huu ligi imekuwa tofauti kwa sababu ligi imekuwa ngumu  ina ushindani mkubwa, timu nyingi zilijiandaa vizuri, ushindani upo hali ambayo timu yoyote inaweza kupata matokeo sehemu yoyote kutokana na jinsi ilivyojipanga  lakini kwa upande wetu nadhani hatukustahili pengine kuwa hapa,” alisema Nsajigwa.

1 COMMENTS:

  1. Nikusaidie tu Yanga ninayoipenda ni ya nne siyo ya tatu. Ipo nyuma ya Singida United yenye pointi 29. Inadhihirisha kuwa haya maneno hayajatoka kwa Nsajigwa. Umeyaandika ukiwa chumbani. Ila asante kwa habari za michezo japo nyingine ni ‘fake’.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic