February 13, 2018



Sare ya bao 1-1 waliyopata Azam FC dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, jana. Imeihakikishia Yanga kubaki katika nafasi ya pili sasa.

Yanga imebaki katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 34 sawa na zile za Azam FC lakini kukiwa na tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Kama Azam FC ingeshinda dhidi ya Kagera Sugar, maana yake ingeiong’oa Yanga kutoka katika nafasi ya pili.

Lakini sasa Yanga ina mchezo mmoja mkononi na kama itashinda mechi ijayo, itafikisha pointi 37 na kuipita Azam FC kwa pointi tatu.

Vita kali inaonekana kuwa katika nafasi ya pili kati ya Yanga na Azam FC ambayo hata hivyo, presha yake imepungua kidogo baada ya Singida United nayo kupoteza dhidi ya Stand United.


Simba inaendelea kubaki kileleni ikiwa na pointi 41 pia ina mchezo mmoja pungufu ukilinganisha na Azam FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic