Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leodeger Tenga amesema ujio wa Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Gianni Infantino si jambo dogo kwa kuwa ni nchi mbili tu za Afrika anatembelea ambazo ni Nigeria na Tanzania.
Infantino anatarajia kuwasili nchini Februari 20 na anatarajiwa kukutana na Rais John Pombe Magufuli.
Tenga aliyewahi kuwa Rais wa TFF, amesema kwa kuwa Infantino ataongozana na marais wa vyama vingine vya soka akiwemo yule wa Caf, litakuwa jambo zuri kuhakikisha Tanzania inaitumia ziara hiyo kwa faida.
“Wameona Tanzania mambo yamebadilika, hata serikali yetu chini ya Rais Magufuli mambo ni tofauti na hakuna mzaha.
“Infantino na Ahmad ni watu wanaotaka umakini mkubwa katika matumizi ya fedha. Wakiangalia wanaona Serikali ya Tanzania nayo inafanya hivyo.
“Wanakuja, tuwaonyeshe sisi ni watu wa soka lakini ni jambo jema sana kama tutaitumia vizuri ziara yao kwa manufaa ya mpira wetu.”
0 COMMENTS:
Post a Comment