February 16, 2018



Kiungo wa pembeni wa kimataifa, Simon Msuva, ameendeleza kufumania nyavu baada ya kuifungia timu yake ya Difaa Hassan El Jadida ya nchini Morocco.

Bao hilo alilifunga juzi Jumatano katika sare ya mabao 3-3 dhidi ya Chabab Atlas KhĂ©nifra katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco ‘Botola Pro’.

Katika mechi hiyo, Msuva aliyetua kuichezea timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Yanga, alifunga bao lake katika dakika ya 42.

Mabao mengine katika mchezo huo yalifungwa na Anouar Jayid dakika ya 82 na Adnane El Ouardy dakika ya 90.

Sare hiyo imefanya Difaa Hassan El Jadida kusogea hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo ikifikisha pointi 25. 


Wiki iliyopita, Msuva aliipigia hat-trick katika ushindi wa mabao 10-0 walioupata dhidi ya Benfica ya Guinea Bissau kwenye mechi ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic