February 20, 2018

PICHA YA MAKTABA: YANGA WAKIWA KATIKA MAZOEZI UWANJA WA UHURU.


Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania, Yanga kitafanya mazoezi yake ya mwisho leo kabla ya kuivaa St Louis ugenini Shelisheli.

Yanga itaifaa St Loiuis katika mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kushinda ile ya kwanza kwa bao 1-0 jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema leo watafanya mazoezi asubuhi kwenye uwanja watakaoutumia katika mechi kesho.

Amesema baada ya mazoezi ya leo, jioni watakwenda uwanjani hapo kuzishuhudia APR ikivaana na timu ya Shelisheli katika michuano ya Kombe la Shirikisho.


“Tutakwenda kushuhudia mechi hiyo na kuwaunga mkono APR kwa kuwa wanatokea katika ukanda wetu,” alisema.

1 COMMENTS:

  1. Ndugu tunashukuru kwa habari nzuri ila jitahidi sana unapotoa habari kama hii kuweka na muda wa mechi utakaochezwa sio siku pekee!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic