May 31, 2018


Na George Mganga

Baada ya kufanikiwa kurejea kwenye Ligi Kuu Bara, uongozi wa klabu ya Coastal Union 'Wagosi wa Kaya' umeanza kupambana kufanya usajili wa wachezaji lakini mambo hayajakaa sawa.

Kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Agustini Mguto, amesema kuwa wameanza kufanya usajili ili kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi.

Licha ya kuanza usajili, Agustino ameweka wazi hali ngumu ya ukata wa fedha ambayo wanakumbana nayo hivi sasa inasababisha mipango yao isiende sawa kama ambavyo ilipaswa.

Mguto ameeleza kuwa tatizo la fedha limeiandama klabu hiyo iliyopanda daraja kucheza ligi msimu mjao kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mawenzi Market ikiwa ni baada ya kushuka msimu wa 2015/16.

Kutokana na hali hiyo ya ukosefu wa fedha, Mguto amesema watajitahidi kufanya jitihada za ili waweze kufanikisha adhma yao ya kufanikiwa kusajili wachezaji ambao watakuwa mhimili wa kikosi msimu ujao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic