June 9, 2018


Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa mapumziko ya wachezaji wake ikiwa ni siku kadhaa baada ya kurejea nchini kutoka Kenya walipokuwa wanakushiriki mashindano ya SportPesa Super Cup.

Kwa mujibu wa Ofisa wa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema wachezaji wote tayari wameshaenda makwao kwa ajili ya mapumziko mpaka watakaporejea tena Juni 25 2018.

Kufuatia likizo hiyo ya muda, wachezaji watarejea tena kambini tarehe tajwa hapo juu kwa ajili ya kuanza maandalizi rasmi ya kuiwinda Gor Mahia FC Julai 18 2018 katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Wachezaji hao wameenda likizo baada ya kushindwa kuiwezesha Yanga kusalia kwenye mashindano ya Super Cup huko Kenya kwa kuondoshwa na Kakamega HomeBoyz FC katika mchezo wa ufunguzi kwa jumla ya mabao 3-1.


2 COMMENTS:

  1. Jamaa wapo hoi kwa matukio na huku wakizidi kujichanganya. Hii ndio yanga ya leo?

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV