June 10, 2018






Na Saleh Ally, Nakuru
SIMBA wametinga katika fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup ambayo inafikia tamati jijini Nakuru hapa nchini Kenya, leo.


Kikosi cha Simba ambacho sasa kipo chini ya Kocha Msaidizi, Masoud Djuma kitalazimika kufanya kazi ya ziada kufikia kile wanachokitaka Watanzania wengi kuivua ubingwa Gor Magia ya Kenya.

Watanzania wengi hasa mashabiki wa Simba wanachotaka ni kuendeleza furaha ya kuiona timu yao inakuwa bingwa na kwenda Everton nchini England kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Everton.

Wanataka Simba iende kucheza mechi hiyo kama sehemu ya heshima, wanataka kuiona Simba ikifanya vema na kurejesha heshima yake. Lakini wako ambao wangetamani hayo yatokee, wapate nafasi nzuri ya kuwazodoa watani wao wa jadi, Yanga.

Pamoja na mipango au matamanio ya wengi kwa kila njia. Ukweli unaonyesha Simba inalazimika kuupanda mlima mrefu hasa ili kufanikisha hayo kwa kuwa Gor Mahia si timu ya mzaha kwa mambo mengi sana.

Uimara:
Michuano hiyo imeanzishwa msimu uliopita, Gor Mahia iliingia fainali na kuwachapa wapinzani wao wakubwa AFC Leopards kwa mabao 3-0 na kufanikiwa kubeba kombe hilo katika ardhi ya Tanzania.


Utaona msimu uliopita walikuwa mabingwa na msimu huu moja kwa moja wakishinda mfululizo wameingia fainali, haitakuwa kazi rahisi.

Fowadi kali:
Gor wanaonekana kuwa na fowadi kali zaidi katika ushambulizi. Angalia mechi mbili, wamefunga mabao matano na wanakwenda fainali kwa mechi zao zote mbili wakishinda ndani ya dakika ya 90.

Simba mambo ni tofauti, hawajafunga hata bao moja katika dakika 90 na wanakwenda kupitia njia ya matuta kwa kuwa mechi zao zote mbili wametoka sare ya bila mabao na wakavuka kwa penalty. Mechi ya kwanza wakiokolewa na kipa wao Aishi Manula na mechi ya pili ikawa kazi nzuri ya wapigaji ambao hawakukosa, ikiwapeleka mbele hadi fainali.

MAana yake, safu ya ulinzi ya Simba inapaswa kujipanga haswaa, maana kama timu imefunga mabao matano katika mechi mbili, haliwezi kuwa jambo la mzaha ingawa hili haliwahi uhakika wa kushinda kwenye fainali, hasa kama Simba watakuwa makini.

Kazi ya leo ya Simba ni ngumu, ni zaidi ya kazi ya jeshi maana ikumbuke Gor imekuwa na kikosi chake kwa muda sasa na kimeanza kupata uzoefu mkubwa wa mechi za kimataifa na pia kina kasi. 

Si kuwakatisha tamaa Simba, lakini lazima wajitume na kujua mechi yao leo itakuwa tofauti sana na mechi zilizopita. Hivyo wachezaji watakuwa na jukumu la kuiamua fainali hiyo kwa umakini na ikiwezekana mapema. Lakini wakizubaa, Gor wataamua.

Mabadiliko:
Simba wanapaswa kubadilika, ni lazima wacheze tofauti na mechi zao mbili. Kama watasubiri penalty, maana yake lazima wataondoka kwa kuwa Gor imeonyesha inaweza kufunga ndani ya dakika 90 kuanzia mabao mawili.

Msimu uliopita ilionyesha, inaweza kufunga hadi mabao matatu katika mechi ya fainali tena ikiwa ni derby, hili nijambo ambalo Simba lazima walipigie hesabu na kubadili kwa kunoa makali ya washambuliaji wao, kwamba lazima wafungwe.

Kuanza kufunga:
Kama Simba wataanza kufunga katika mechi hiyo, basi watakuwa wamejiwekea ahueni kubwa sana ya kuufanya mchezo kwao upangike vizuri na presha kupungua.

Lakini kama wataruhusu kufungwa na hasa katika dakika za mwanzoni au kipindi cha kwanza, watatengeneza au kuruhusu presha kubwa sana ambayo baadaye inaweza kuwaondoa mchezoni na kusababisha kufungwa mabao hata zaidi ya mawili.

Hii inaweza kuwa hivyo kwa kuwa Simba haijafungwa hata bao moja katika mechi mbili na imefika fainali kama ilivyo kwa Gor. Lakini Gor wana advantage kwa kuwa hawakufungwa lakini wamefungwa.

Kwa maana ya takwimu, Simba inakutana na timu bora zaidi ya michuano hiyo kwa msimu huu hadi sasa. Kulibadili hilo ni lazima kuifunga na kuing’oa.

Kulinda:
Simba na Gor ndiyo timu zenye rekodi nzuri ya kutofungwa hata bao moja ndani ya dakika 90. Kama Simba itafanikiwa kulinda kwa dakika 90 zote, pia litakuwa jambo zuri lakini si salama sana kwa kuwa halina uhakika.

Lakini kama itahakikisha haifungwi na inatafuta kufunga. Halafu mechi ikaisha kwa dakika 90 bila bao, basi hofu au presha itakuwa kwa Gor ambao walizoea kila mechi kumaliza ndani ya dakika 90 na wanaweza kutengeneza nafasi ya ubora kwa Simba katika suala la penalty na wakashinda.

Kagere:
Meddy Kagere, raia huyu wa Rwanda mwenye asili ya Uganda, amefunga mabao matatu lakini mawili ni ya vichwa vya mtindowa kuchomoza ambavyo viliwashinda mabeki wa JKU na Singida United. Hakika Simba wana upungufu wa watu wepesi kwa kuwa waliruhusu Kariobang Sharks kupiga vichwa vingi sana. Kagere akiachiwa nafasi zile, basi wajue anatumbukia nyavuni.

Mfumo:
Kama inawezekana iko haja ya Djuma abadili mfumo. Ule wa mechi mbili na hasa ya kwanza wa Kocha Mfaransa, Pierre Lechantre ambaye amevurumishiwa vifaa arejee kwao, ulikuwa ni wa ulinzi mkubwa.

Simba ilicheza katika zone yake kwa muda mwingi. Kwa Gor, wakifanya hivyo, hatari zitakuwa nyingi kwao mfululizo na mwisho watajikuta wanaachia baada ya kubana sana.

Kikubwa kinachotakiwa, Simba nao kufanya mashambulizi makali yatakayowapa Gor presha na kulazimika kuimarisha ulinzi na kupunguza mashabulizi kwenye lango la Simba.

Kama Kagere na Jacques Tuyisenge nao watarejea kusaidia, basi maana yake hakutakuwa na presha kubwa katika lango la Simba nah ii takuwa ni kutengeneza usalama wakati ukiangalia wapi pa kufanya mipango ili kumaliza mchezo.

MECHI

SIMBA:
Simba 0-0 Sharks
 * (Penalti 3-2 Simba kashinda)

Simba 0-0 Homeboyz
 * (Penalti 5-4 Simba kashinda)

GOR MAHIA:
Gor Mahia 3-0 JKU
Gor Mahia 2-0 Singida United





2 COMMENTS:

  1. Pengo la akina Okwi lipo dhahiri na hata kwenye ligi kuu walikuwa wakikosekana simba ilitaabika. Sasa hawa vijana waliosajaliwa sasa hatuwezi kuwalaumu Kwanza hawana uzoefu wa mechi za kimataifa lakini kwa upande mwengine ni advantage au faida kwa hawa vijana kungara hapa waache uoga tu kwani opportunity is hardly to come twice. Yaani bahati sio rahisi ikajirejea tena na tena na inapokuja mtu anatakiwa kuwa shapu kuitumia kwa faida. Kiuhalisia Simba ina nafasi zaidi kuliko Gormahia katika mchezo wa kesho kushinda tofauti labda na watu wanavyofikiria na inaweza ikawa mechi rahisi sana kwa simba kama kutafanyiwa marekibisho katika safu ya ushambuliaji . Timu alizokutana nazo Gormahia ni nyepesi zaidi za zile alizocheza nazo Simba. Lakini masuala ya safari na uchovu na ugeni wa mazingira ulichangia kwa Simba kutocheza vizuri katika mechi zilizopita na ndio maana ukaoana mechi ya pili wakenya wengi walishangaa kiwango alichoonesha Simba na ni imani kubwa kesho wakenya watapata sapraizi nyengine kubwa kutoka kwa Simba ila akina Salamba na kaheza na Mo Rashidi kama watabahatika kupewa majukumu ya ufungaji kesho basi wajue wanauwezo mkubwa tu wa kufanya hivyo kuliko hata yule Kagere ni kujiamani tu kwanza wanafaida kubwa mbele ya Gormahia ya wao kuonekana ni wachezaji wa kawaida tu kulinganisha na akina Boko na Okwi lakini Mbwana Samata aliwapa somo TP Mazembe licha ya kuonekana wa kawaida na kilichotokea baadae kwa Samata ni historia. Kwa hivyo vijana hiyo nafasi ni hadimu na mnatakiwa kuitumia vizuri Piga Ua na hapana shaka uwezo mnao.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic