June 18, 2018






Igawa kumekuwa na kukwepa maneno hapa na pale, imeelezwa kuwa Real Madrid imekuwa ikifanya juhudi ikiwa ni pamoja na kuwatumia wachezaji kadhaa kuhakikisha wanamnasa Neymar.

Wachezaji wanaotumika ni wale raia wa Brazil walio katika kikosi hicho cha mabingwa wa Ulaya lakini hata wale wakongwe waliowahi kuitumikia.

Marcelo na Casemiro ni kati ya wanaotumiwa na Madrid kuhakikisha inamnasa Neymar kutoka PSG na kumrejesha Ufaransa lakini safari hii Madrid.

Neymar aliwahi kutua Madrid akiwa kinda lakini baadaye akarejea nchini Brazil na kuendelea na timu yake ya Santos ambayo ilimkuza kisoka, kumfaya awe maarufu kabla ya kujiunga na FC Barcelona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic