June 9, 2018


Na George Mganga

Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amewataka Yanga kutengua ombi lao ndani ya saa 48 la kutaka wasishiriki michuano ya Kombe la KAGAME inayotarajia kuanza Juni 28 2018 jijini Dar es Salaam.

Hatua ya imekuja kufuatia uongozi wa klabu hiyo kutuma barua inayoeleza kuomba kujitoa ili kuwapa wachezaji wake mapumziko kwa ajili ya kuja kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC.

Karia amefunguka kwa kuwapa Yanga saa 48 kwa maana ya siku mbili kuanzia leo kutengua kauli hiyo akieleza kuwa hata Gor Mahia ambao wapo kundi moja CAF pamoja na Rayon Sports wamethibitisha kushiriki.

Rais huyo ameongea kauli hiyo kwa msisitizo akiamini Yanga wanaweza kubadilisha maamuzi hayo aliyosema hayana mashiko ili kuungana na wenzao Simba ambao wamepangwa kundi moja kushiriki mashindano hayo yatakayomalizika Julai 13.

Yanga walituma barua hiyo TFF juzi wakiomba kujiondoa kwenye mashindano hayo kwa lengo la kuwapa wachezaji nafasi kujiandaa katika michuano ya CAF ambapo Julai 18 Julai 2018 watacheza na Gor Mahia huko Kenya.


7 COMMENTS:

  1. Lakini kwanini Raisi Karia anakuwa mkali kupitiliza kiasi kwa Yanga? Tangu yanga ikumbwe na misukosuko hatuja msikia kusema au kuwasaidia kwa lolote lile. Sina uhakika katika masuala ya sheria lakini kama Yanga wanahisi hawana uwezo wa kushiriki mashindano hayo vipi walazimishwe washiriki kwa lazima?
    Timu ya Taifa haina mwelekeo wowote ule unaojulikana hata kidogo, hata kocha haina lakini hilo halioneshi kumkera muheshimiwa Karia. Kwa kweli tuwe wawazi kabaisa TTF haijapata watu wa kuiongoza bado na ni dhahiri soka letu letaendelea kuzorota licha ya sasa Tanzania kujaliwa rundo la wachezaji mahiri vijana wenye uwezo wa kupindua meza na kulipaisha soka letu lakini vipaji hivi vitapotelea mbali na kuiacha Tanzania ikiendelea kushikia mkia kila siku.

    ReplyDelete
  2. Dawa ya Jeuri Kiburi...Peleka Yanga B. TFF wao wanaangalia zaidi mapato, hawako kwenye kusaidia clubs za bongo kufanikiwa kwenye mashindano.

    ReplyDelete
  3. Hana mamlaka ya kuipangia ni kuingilia ya ndani ya Timu husika. Usilete ushabiki na uzandiki wako hapa. Nahisi unapata furaha sana kuona timu ina-struggle bila msaada wowote. Timu ilienda Algeria bila hata mwakilishi. Yanga hawaangilii hao Gor Mahia wapo kwenye kundi au la..Yanga imejitetea yenyewe. watu hawafanyi hata mazezi...timu ikaenda Mbeya...ntie mkaa kimya...Tunajua malengo yenu yalikuwa nini...ndio maana ukaona viongozi wamekaa kimya. Kagame ni mashindano yasio ya lazima....wacha wengine nao wacheze. Kama mlikuwa na lengo lenu basi hapa mmekula ya chuya. Miaka mitatu mfululizo hakuna kujenga timu..timu inapambana...sasa acha timu ijengwe upya. Kwa kauli moja...timu haitashiriki Kagame...waache Mtibwa au Singida wacheze

    ReplyDelete
  4. Haya ndio waliyokuwa wanayoyatafuta Yanga na Kisa ni kutishwa na Haji Manara. Yanga isijitie unyonge hata ikabidi kukaripiwa kama mtoto mdogo. Yanga ni kati ya timu maarufu sana ukana wa mashariki ya Africa. Alilotamka Manara ni utani wa kawaida tu kama vile mlivoizomea Simbs

    ReplyDelete
  5. TFF wana malengo gani na michuano ya Kagame? Tunapeleka timu ili zikashiriki au tunapeleka timu zikashindane? Yanga wamejitathmini na wamegundua hawana timu ya kushindana, unawezaje kuwalazimisha washiriki? au timu inavyofungwa na kutia aibu, TFF wanafaidika na nini? Kila mtu anajua kuwa wachezaji yanga hawajalipwa mishahara wala posho zao kwa kipindi kirefu,kila mtu anajua kuwa Yanga hata ligi wamemaliza kwa kubahatisha hadi wanakula kwa mama ntilie kwa kukusa hela za maandalizi,kila mtu anajua kuwa sasahivi yanga haina kocha maana Nsajigwa vyeti vyake havimruhusu kukaa benchi kama kocha mkuu hata kwenye VPL,Wachezaji wengi wamegoma na timu imebaki na kikosi kidogo tena kisicho na ubora, wakati timu inajipanga ili iweze kurekebisha makosa kwa ajili ya michuano ya CAF; TFF inawalazimisha eti wakashiriki kagame na si kushindana. Ndo hapo najiuliza hii TFF haiyaoni haya? au wanafaidika na nini kuona Yanga inafanya vibaya? Mbona kuna timu nyingi nzuri zenye uwezo wa kushindana? kwanini wasipeleke hizo? Binafsi naamini SIMBA, AZAM, SINGIDA UNITED, MTIBWA ni bora kuliko Yanga ya sasa.

    ReplyDelete
  6. Niliambiwa wakati wa uchaguzi wa TFF kuwa uongozi umeshatengenezwa na wala si kuchaguliwa lengo kubwa likiwa ni kulipiza visasi na haya ndo tunayoyaona.TFF chini ya Karai na CECAFA chini ya Misonyo wana chuki za dhahiri dhidi ya Yanga.Kuthibitisha hili rejeeni kauli ya Misonyo siku alipokuwa anatangaza makundi ya timu alipoonoekana akiwalenga watu na timu fulani kuwa wamekuwa wakiikwamisha CECAFA utadhani muhimili wa CECAFA ni Yanga.
    Mi huwa najiuliza hivi bila ya Yanga hakuna CECAFA???

    ReplyDelete
  7. Hatuangalii na kuchagua timu gani zishiriki, yanga alikuwa bingwa, na hata ingehitajika timu moja kushiriki kutokana Tanzania, Nafasi Hiyo ilikuwa ni ya yanga. Tatizo ni LA wapangaji wa makundi wakilenga mapato LA kuipanga yanga kundi moja na Mnyama

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic