June 12, 2018





Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Kenya, Gor Mahia, Dylan Kerr amesema yuko tayari kurejea Simba, lakini ametoa masharti.

Kerr amesema anaweza kurejea na kuifundisha Simba ikiwa kama rundo la viongozi waliopo sasa wataondolewa.

Kerr ameiambia SALEHJEMBE mjini Nakuru, Kenya kwamba aliamua kuondoka Simba kutokana na matatizo lukuki yaliyosababishwa na viongozi.

“Bado baadhi yao wapo, ni watu ambao wanaingilia kazi za makocha, hawajui wanalolifanya na hakuna kocha anayeweza kuja akafanikiwa.

“Simba ndiyo, naipenda na kama kurudi inawezekana. Lakini ni lazima uongozi wa sasa kama ni wamiliki, wawaondoe watu hao.”

Kerr ameiwezesha Gor Mahia kuchukua ubingwa wa Kombe la SportPesa Super Cup kwa mara ya pili mfululizo, safari hii wakiifunga Simba kwa mabao 2-0 katika mechi ya fainali.

9 COMMENTS:

  1. Yes, Kerry is an excellent coach that's why he succeed to lead Gormahia to country's championship and Sprtspesa for two consecutive years with vast margins. He is a polite gentleman working quietly without making any noise. Harassment in the team by leaders with personal interests have been the key obstacles that made key team's stars quit Simba, therefore if approached, he should not turn down the offer because those culprits have almost vanished, leaving Simba firm and secured under the new owner's leadership of Billionaire Mo. The team's future is already bright and prosperity is the ultimate goal. Mo is a very organized leadr. He can chop down the tree within one hour, but he would always spend the first half hour sharpening the axe.

    ReplyDelete
  2. Kerry anaweza kurejea kufundisha simba na akachemka.Ni makocha wachache sana Duniani wenye uwezo wa kupeleka mafanikio kila mahala wendapo kufanya kazi. Na kama ni makocha basi kerry ni kocha wa kawaida sana kwani sidhani kama SIMBA ingelikwenda Kenya full mziki akina Asante kwasi,Emanuel okwi alafu Kerry angebakia Salama lakini kwa sasa Kerry haki yake kuchonga.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Issue siyo kuifunga GorMahia angalia uchezaji wa o walivyo na nidhamu ya mchezo kitu kama hicho alianza kukifanya Lechantre midomo midomo ikaanza Simba ilikuwa ngumu kufungika hata ikicheza vibaya

      Delete
  3. Very nice detailed comment

    ReplyDelete
  4. Wee wa ajabu sana una maana simba bila Okwi na Kwasi haijakamilika, poor primitive

    ReplyDelete
  5. Naiusia Simba ifanye hima kubwa kumnas.a Kerr na Kagere wake bila ya kupoteza wakati

    ReplyDelete
  6. SIMBA iliwakosa Asante kwasi,Nicholasi Gayani,James kotei Juko Murshidi,Emunueli Okwi,Mavugo. JOHN BOKO.Yaani kwa kiasi fulani Gormahia walicheza na Simba B. Yanapokuja mashindano ya kimataifa basi hapo ndipo mchecheto na madhaifu ya wachezaji wa kitanzania utakopoyaona. Na ndio maana tunasema kwa Simba kuwakosa wachezaji wake wote wa kigeni katika mashindano yale ndio sababu ya kuonekana timu ya kawaida sana. Wewe kweli mchezaji namba mbili na namba tatu wanaofuatia kwa ufungaji wa mabao ligi kuu bara katika mechi tatu wanashindwa kufunga hata bao la kuotea? Halafu tayari unaweza kuona washajivisha ustaa? Mavugo licha ya mapungufu yake kama angekuwepo pale nakuru walai asingekosa kufunga. Hwawa vijana Kwanza ni walaini mno na wanatakiwa kufahamu hilo na wanatakiwa kubadilika haraka la sivyo wataishia kuchoma mahindi pale SIMBA na hasa baada ya simba kuamua kuleta watu wa kazi zaidi kutoka nje ya Tanzania baada ya kujiridhisha kuwa hawa vijana bado. Pale beki kama wangekuwepo Juko na kotei basi Kagere angefurahi sio kama nawaponda wachezaji wetu wa kitanzania ila mechi za kimataifa ni tatizo nadhani ni uoga na uoga huo ndio unawafanya kutothubutu kujaribu kucheza nje.

    ReplyDelete
  7. Na kwakweli sina uhakika kama Simba nia yao ilikuwa kuwapa nafasi wachezaji wa nyumbani hasa vijana katika mashindano ya sports pesa ili kujitnagaza zaidi kwani ni jambo zuri vile vile kuwapatia fursa wachezaji wazawa kwa uzoefu zaidi kwani kuisha kwa mafuta sio mwisho wa safari tusiwakatishe tamaa..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic