June 20, 2018


KITANDU AKIWA NA NDEMLA


Mambo yanaweza kumnyookea mshambuliaji chipukizi wa Simba, Moses Kitandu ambaye sasa safari ya kuanza maisha nchini Kenya, inanukia.

Kitandu inaonekana ameivutia klabu ya Nakumatt ya Kenya ambayo imeweka wazi kwamba inamtaka.

Kitandu ambaye ni miongoni mwa wachezai vijana wa Simba ambao msimu wa 2017/18, walipandishwa kutoka timu ya vijana ya alikuwa kwenye kikosi cha timu hiyo kilichomaliza nafasi ya pili kwenye michuano hiyo ambayo bingwa wake alikuwa Gor Mahia.

Kitandu alisema yupo tayari kujiunga na timu yoyote ikiwemo hiyo Nakumatt ambayo imeonyesha nia ya dhati ya kumhitaji.

“Ni kweli kuna timu kutoka Kenya ambayo ni Nakumatt imeonyesha nia ya kunihitaji nijiunge nayo, nitafanya hivyo endapo tu watafuata utaratibu kwa kuongea na viongozi wangu wa Simba kwani kwa sasa nipo kwenye mazungumzo na klabu yangu baada ya mkataba kumalizika.

“Mbali na hiyo, kuna timu zingine zinazoshiriki ligi kuu ambazo ni Singida United, KMC na Coastal Union ambazo nazo pia zinanihitaji, kikubwa ninachoangalia ni maslahi yangu pamoja na ruhusa kutoka timu yangu ya Simba,” alisema Kitandu.

Kitandu alipata nafasi ya kuonyesha cheche zake wakati wa michuano ya SportPesa Super Cup iliyofanyika Nakuru nchini Kenya.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic