June 9, 2018


Uongozi wa Azam FC kupitia kwa Afisa Habari wake, Jaffer Idd Maganga, umesema kuwa mchezaji wake aliyesajiliwa kutoka Yanga atakosekana dimbani kwa muda wa miezi miwili.

Maganga ameeleza hayo mara baada ya mchezaji huyo kuwasili leo nchini akitokea Afrika Kusini baada ya kufanyiwa vipimo vua afya katika hospitali ya St, Vincent Parrot iliyoko Cape Town.

Ofisa Habari huyo amesema kuwa, kwa mujibu wa taarifa za Daktari, Mwanandi Mwankemwa, ameeleza kwamba Ngoma amegundulika kuwa na tatizo la uvimbe katika goti lake la kulia.

Mwankemwa amefafanua kuwa goti hilo limeonekana kuwa na uvimbe kwa ndani ambao ulikuwa unaelekea kupona hivyo itampasa afanye mazoezi mepesi kwa ajili ya kuliweka sawa na hatimaye aweze kupona vizuri.

Kutokana na hali hiyo, Maganga amesema Ngoma atapaswa kupumzika kwa muda wa miezi miwili na wiki moja na sasa atakayokosa mashindano ya Kagame CUP yanayotarajia kuanza mwisho wa mwezi huu.

2 COMMENTS:

  1. Waliokuwa wakimfikiria Ngoma kuwa anakacha tu michezo haumwi, jee si ubaya wa bure? Mwenyewe Ngoma aliwahi kujitetea kwa kusema ...hivi kuna mchezaji anapenda kukaa tuu bila kucheza mpira kwa zaidi ya miezi 6?... lakini walimwengu sisi shida ... hatukumuamini. Nawapongeza AZAM kwa moyo wa huruma na kumpatia matibabu mchezaji huyu.

    ReplyDelete
  2. Tehteh, drama. Eti uvimbe uliokuwa unaelekea kupona, afanye mazoezi na kuwa nje wiki 9.
    Wenye akili tulisha jua mwisho wa sinema hii.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic