June 8, 2018




Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Mfaransa Pierre Lechantre, jana alishindwa kikiongoza kikosi chake wakati wa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Kakamega HomeBoyz FC.

Mfaransa huyo aliwatazama vijana wake wakipigania ushindi akiwa jukwaani sambamba na Mwalimu wa viungo, Aimen Habibu huku Msaidizi Masoud Djuma akiwa kwenye bechi la ufundi.

Taarifa ambazo uongozi wa Simba umegoma kuziweka wazi, imeelezwa kuwa Lechantre aliamua kukaa jukwaani ikielezwa alisusa kukaa kwenye benchi akidai apewe mkataba mpya.

Ikumbukwe kuwa Lechantre aliwasili nchini mwezi Januari mwaka huuu na kusaini mkataba wa miezi 6 unaomalizika mwezi huu.

Licha ya maamuzi hayo kutokaa na benchini jana, Mfaransa huyo anaelezwa kuwa na mahusiano mazuri na ya karibu zaidi na Aimen ambaye ni Mwalimu wa mazoezi ya viungo, tofauti na Djuma ambaye ni msaidizi wake.

Uwepo wa tukio hilo unaleta sintofahamu kubwa ndani ya bechi hilo la ufundi Simba ambapo hatima ya Mfaransa huyo itajulikana mara baada ya mkataba wake kumalizika.

1 COMMENTS:

  1. Djuma mbona safi tu anatutosha. Wazungu waende tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic