June 16, 2018


Baada ya Kamati Maluum ya Mpito iliyoteuliwa na uongozi wa Yanga katika Mkutano Mkuu wa klabu uliofanyika hivi karibuni, baadhi ya wanachama wameibuka na kusema kuna namna inafanyika kuhusiana na fedha za usajili.

Ramadhani Kampira ambaye ni Mwanachama wa Yanga na Mwenyekiti wa wachezaji wa zamani wa klabu hiyo ameeleza kuwa kuna namna inafanyika juu ya fedha za usajili kutotumiwa na walioundiwa kamati.

Kampira amesema kuwa, Kamati ya Mpito ambayo ipo chini ya Abass Tarimba imenyimwa mamlaka ya kufanya usajili na badala yake imepewa majukumu ya kutafuta fedha ili ziufikie uongozi wa Yanga.

Mwanachama huyo amesema anapinga suala hilo huku akieleza inabidi Kamati hiyo ifanye kazi yake na si fedha kuwasilishwa kwa Clement Sanga ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa klabu.

Mbali na Kampira, Mwanachama mwingine anayejulikana kwa jina la Waziri Jitu, naye ameeleza akisema inabidi Sanga aiachie Kamati hiyo ifanye maamuzi yake na si kuanza kuipangia majukumu.

CHANZO: RADIO ONE

1 COMMENTS:

  1. Kuonyesha kutowaamini Viongozi wetu wa juu sio jambo jema.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic