June 16, 2018


Mchezaji wa klabu ya Yanga, Juma Mahadhi amesema kuwa bado hajamaliza mkataba na timu yake hivyo bado ni sehemu ya timu hiyo mpaka sasa.

Mahadhi aambaye alisajiliwa kutoka Costal Union iliyorejea tena katika Ligi Kuu na tayari kucheza msimu ujao, ilikuwa inaelezwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji ambao wanaweza wakaondoka Yanga kutokana na mkataba wake kumalizika.

Taarifa hizo amezipinga mchezaji huyo akisema si za kweli na akiwaomba wapenzi na wanachama wa Yanga kuendelea kuipa sapoti timu yao.

Kiungo huyo yupo likizo hivi sasa kabla ya kurejea tena kambini hapo baadaye baada ya wachezaji wote wa timu kupewa mapumziko.

Wachezaji wa kikosi cha Yanga kwa ujumla watarejea tena kambini mwezi ujao kwa ajili maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic