June 9, 2018


Timu ya Golden State Warriors imetwaa ubingwa wa ligi ya mpira wa kikapu Marekani (NBA) baada ya kuendeleza ubabe dhidi ya wapinzani wao Cleveland Cavaliers kwa kuwashinda mechi mfululizo 4-0 baada ya kutoka na ushindi wa mwisho wa pointi 108-5.

Katika  mchezo wa kuamua uliopigwa asubuhi ya kuamkia leo, Stephen Curry alitupia mara 37 ambapo Kevin Durant alitupia mara 20.

Hatua hiyo imekuwa ya majonzi makubwa kwa Cavs ambao wamepoteza michezo yao minne ya mwisho dhidi ya Golden.  Vilevile, nyota wa Cavs, Le Bron James, ambaye huenda alicheza mhezo wake wa mwisho kwa timu hiyo, alifichua kwamba alicheza akiwa ana maumivu kwenye mkongo wake.

Kutokana na Golden kucheza vyema, wachezaji wao waliokuwa benchi walianza kushangilia mapema, sekunde chache kabla ya mchezo kwisha, wakiwa na uhakika wa ushindi na kutwaa ubingwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV