June 9, 2018


Na George Mganga

Mshambuliaji wa kimataifa kutka Benin, Marcellin Koukpo amewasili jana usiku akitokea nchini kwao na kupokelewa na Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten.

Koukpo ambaye alikuwa kwenye mazungumzo ya muda mrefu na uongozi wa Yanga ametua leo tayari kutia kandarasi na mabingwa hao mara 27 wa ligi kuu nchini.

Koukpo ambaye alikuwa akiichezea Les Buffles FC ya huko Benin inaelezwa tayari ameshamalizana kwa kila kitu na Yanga na atasaini mkataba wa miaka miwili.

Taarifa za ndani zinasema Koukpo atakabidhiwa jezi namba 11 ambayo alikuwa akiichezea Donald Ngoma baada ya kuondoka kutimkia Azam FC.

2 COMMENTS:

  1. Jambo jema hilo ataisaidia timu kufanya vizuri

    ReplyDelete
  2. Inapendekeza atatusaidia kama scouting ilifanyika vizuri.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV