BAADA YA KUISAIDIA YANGA, MWIGULU NCHEMBA AWAKARIBISHA SIMBA KWA MSAADA ZAIDI
Baada ya kuwasaidia Yanga kupata baadhi ya wachezaji kwa ajili ya msimu ujao, Mlezi wa klabu ya Singida United, Mwigulu Nchemba, amezikaribisha Simba na Mtibwa kwa ajili ya msaada zaidi.
Nchemba amesema yeye ni mdau wa soka na yupo kwa ajili ya kuzisaidia klabu ambazo zinapitia wakati mgumu kwa kuwa anapenda zifanikiwe.
Kiongozi huyo ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, amefunguka na kusema kuwa Yanga walichelewa kuhitaji msaada kutoka kwake hivyo walipaswa kumpa taarifa mapema awasaidie zaidi.
Aidha amezigusia Simba na Mtibwa Sugar ambazo zinajiandaa kushiriki mashindano ya kimataifa kuanzia Disemba mwaka huu kuwa kama zinahitaji msaada wa wachezaji vema wakazungumza naye.
Nchemba amewataja Simba kutokana na ugumu wa mashindano ya CAF kutokana na maelezo yake kuwa anaweza akawasaidia wachezaji wa kimataifa ili kukipanua zaidi kikosi chao.








Kubwagwa kubaya.... Ona Sasa mzee wa watu anatapatapa hujui kipi aongee
ReplyDeleteYanga bado wanaitaji msada kumlipa rostand mbona hujamaliza mkuu wa yanga
ReplyDeleteAibu hiyo.
ReplyDeleteAtoe msaada Simba???? Abaki huko huko simba sio tuko vizuri..
ReplyDelete