July 24, 2018


Na George Mganga

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amewapa Simba siku 75 pekee ili kufanya uchaguzi kuwapata viongozi wengine watakaoiongoza klabu kwa miaka minne ijayo.

Karia ameongea hayo alipoitisha kikao na Waandishi wa Habari kunako makao makuu ya Shirikisho hilo yaliyopo Karume, Ilala, Dar es Salaam na kusema kuwa Kamati ya Uchaguzi TFF imemfikishia Karia taarifa za kuitaka Simba ifanye uchaguzi huo.

Karia ameeleza kuwa kwa kawaida siku ambazo hutolewa ni 60 pekee lakini amewaongezea zingine 15 ili kufanya maandalizi kuelekea uchaguzi huo ambao ni kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2014.

Hivi karibuni viongozi wa Simba waliiomba TFF iwape muda ili kuifanyia mabadiliko katiba yao mpya ambayo ipo kwa Msajili wa Serikali ambayo inaendana na mfumo mpya wa mabadiliko ambao klabu inaelekea kuukamilisha.

Wakati Karia akinena hayo, kikosi cha Simba hivi sasa kipo nchini Uturuki kwa kambi ya wiki mbili kujiandaa na tamasha la Simba Day pamoja na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

Kikosi hicho kinafanyia mazoezi yake katika Uwanja wa milima ya Kartepe nchini Uturuki ambapo kimefikia katika Hotel ya Green Park Kartepe Resot & Spa.

2 COMMENTS:

  1. Muhimu viongozi waliopo madarakani hivi sasa wanadi sera yao ya maboresho makubwa waliyofanya ndani ya klabu ikiwa ni pamoja na kutengeneza kikosi imara kabisa kilichochukua ubingwa wa VPL kusajili wachezaji wengi na mahiri kwelikweli, kuleta mfumo wa kuiendesha klabu kwa mfumo wa kampuni, kupeleka timu Uturuki kuweka kambi ya wiki mbili kujiadaa na VPL, kuleta makocha bora kabisa, baada ya mafanikio hayo wanachama tunataka nini? Viongozi waliopo sasa madarakani wapewe ridhaa ya kuendelea kuongoza klabu kwa miaka 4 ijayo huu uchaguzi utakuwa muda mfupi sana. Tusiharibu timu muda huu kwa kuingiza viongozi wanaogeuka nyuma kuwa jiwe. Simba lazima tuoneshe mfano mzuri kwenye hili.

    ReplyDelete
  2. Namfagilia kaimu Rais wa sasa wa klabu Salim Abdallah "Try Again" kugombea Urais ili aendeleze mfumo wa mabadiliko na hadi kufikia hapa leo si haba.Mwanzo ni mgumu kwani tumesikia na tutaendelea kusikia kejeli, maneno ya kukatisha tamaa, kupikwa majungu, hujuma.Pia nawapongenza kamati ya utendaji ya Simba kwa ushirikiano walionyesha na bila ya kuwasahau walio kwenye matatizo kina Aveva, Nyange, Hans Pope.Wanachama, washabiki wa klabu yetu ya Simba tuendelee kushikamana na kuwaunga mkono viongozi na mwekezaji mkuu na hata kuwakaribisha wawekazaji wengine kununua hisa 51% za wanachama.SIMBA NGUVU MOJA!!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic