July 27, 2018



NA SALEH ALLY
NIMEZUNGUMZA sana kuhusiana na klabu kongwe ya Yanga kuendelea kulia kuhusiana na mfadhili wao au Mwenyekiti wa zamani, Yusuf Manji.

Kwa wanaoelewa wanajua umuhimu wa Manji ulivyokuwa na nimefafanua mara kadhaa kuhusiana na hilo.

Raha kubwa kwangu ni kwa kuwa nilisema kabla ya Manji kuondoka kwa wale waliokuwa wakimpigia kelele kwamba yeye si muhimu, Yanga itajiendesha vizuri hata aondoke leo na kadhalika.

Kama hiyo haitoshi nikawakumbusha hata baada ya Manji kuondoka, hasa baada ya maisha kuanza kuwa magumu na wengi kuanza kumlilikia.

Kwa wale wanaokumbuka, nilikumbusha tena baada ya baadhi ya viongozi kuanza kujiondoa. Viongozi hao ndiyo waliosema Yanga ina uwezo wa kujiendesha bila ya shida na waliona Manji hakuwa muhimu sana.

Lakini baadaye kilichotokea, wakakimbia na leo tunaiona Yanga ikiendelea kusota wao wakiwa kando. Wamekaa kimya na zile kelele na majigambo dhidi ya Manji hayapo tena. Kinachoendelea ni Yanga kupambana kwa nguvu wakimuangukia Manji arudi.

Waka kila haki ya kufanya wanachokitaka, lakini mambo yako hivi. Manji anaweza kurudi kama watafanikiwa lakini kuna haja ya kujiuliza, itakuwa milele?

Unaweza pia ukajiuliza kuwa kama Yanga wanamlilia Manji, kipi hasa wamekosa au kipi hasa yeye alikuwa anafanya hadi wao wanataka leo arejee.

Binafsi najua ni mambo mawili makubwa Manji aliyafanya ingawa yanaweza yakawa na nyongeza ya mambo zaidi ya mengine matano. Hakika Manji alikuwa imara katika suala la mipango na usimamizi wa fedha.

Pili Manji alihakikisha matumizi ya fedha yanakwenda sahihi na alikuwa na uwezo angalau wa kuikopesha au kuisaidia Yanga mambo yanapokwenda vibaya na baadaye akarejeshewa.

Kuna mambo wanayaweza Yanga katika hayo na mfano, Yanga kama klabu kubwa inapaswa kuwa na fedha. Kwa kuwa kwa wadhamini  na mapato kidogo yamilangoni, Yanga sasa wanaingiza zaidi ya Sh bilioni moja.

Kama Yanga wanaingiza kiwango hicho, wanashindwa vipi kupamga mipango madhubuti ya kuingiza fedha nyingi zaidi ili kuendelea kujiendesha?

Wafanyabiashara au makampuni mangapi yangependa kujitangaza kupitia Yanga. Nani ndani ya Yanga anafanya kazi hiyo kwa ufasaha akipita huku na kule kujaribu kuyashawishi kwa utaalamu ambao utawafanya watoe fedha zao.

Yanga inapaswa kuwa na kitengo bora cha masoko. Maana wadhamini wanapaswa kushawishiwa kwa kupewa ‘proposal’  nzuri inayoonyesha watafaidika au kuuza vizuri bidhaa zao.

Yanga ina mdhamini mmoja tu kifuani. Kunanafasi nyingi katika jezi zao ambazo ziko wazi na zingewaingizia fedha na kuondoa ukata unaowakabiri kwa kipindi hiki hadi kuifanya timu ipoteze sifa yake iliyokuwa imefikia.

Lazima kuwe na ubinifu badala ya kulalamika tu kila kukicha na kulialia. Viongozi walio ndani ya Yanga waonyeshe wanaweza kujikwamua kabla ya Manji au hata ikishindikana kwamba hawezi kurejea.

Suala la Manji kwa Yanga lilipaswa kuwa plani B baada ya uongozi kuwa umepambana na kupata fedha kupitia udhamini na kadhalika.

Yanga kuendelea kulalamika, kulia hawana kitu hii ni aibu na hili ni jambo la utafakari. Tatizo jingine ninaloliona ni kila mmoja kujiona ni klabu yake, ana amri juu yake, hivyo kupoteza haki ya wale wanaopambana.

Anayepambana anaweza kuwa na mipango inayochukua muda. Mwingine anaweza kuona inachelewa naye akafanya tofauti kwa kuwa tu ni klabu yake.

Wakati wa Manji, hakuna aliyekuwa anaweza kuingilia na heshima ya muongozo ilikuwa juu ndiyo maana Yanga ikabadilika na kufanya vizuri.

Yanga punguzeni kulialia. Klabu ya Yanga ina heshima zake ni kubwa na mtaji. Fanyeni jambo.



4 COMMENTS:

  1. tatizo la klabu zetu zinaendeshwa kienyeji na pia viongozi wako kwa ajili ya masilahi yao Timu kama barcelona na Mdrid ni timu za wanachama lakini hakuna timu yoyote duniani ambazo zinaweza kushindana nazo pale zinapotaka kusajili wachezaji ingawa kuna timu zimenunuliwa na matajiri wa kiarabu wenye pesa za mafuta.
    Hivi vilabu vyetu vinapaswa kufanya kazi kwa weledi wakati nafasi za mweka hazina, katibu na ofisa habari zinatakiwa kuwa za kuajiliwa bado vilabu hivi havifati taratibu za ajira kwani nafasi hizi zimekuwa zinatolewa kienyeji hata wakisema wawe na maafisa masoko bado timu hizi hazitatafuta watu wenye uwezo .
    TFF ambayo ilipaswa kusimamia swala hili nao wanafanya hivyohivyo juzi tumeona katibu wa tff akiteuliwa badala ya kupitia mchakaato mzima wa kumpata vyombo vya habari vimenyamazia swala hilo na kuliona kama la kawaida

    ReplyDelete
  2. Unaweza ukawa Sawa na mawazo yako tatizo timing haikuwa sahihi. Yang a kama taasisi wala wapenzi na wanachama hawakujiandaa na kuondoka Manji Kwa Ghafla

    Bata hiyo wako kwenye process tu na baada ya muda watKubaliana na Hali halisi na watajipanga

    Tatizo kubwa LA Simba na Yanga ni kubwa na fikra za utegemezi na mawazo Mando. Lazima kubali mtazamo. Hata simba pamoja na uwekezaji WA MO Lazima wajiongeze Maana hata matajiri huwa wanapata Fatigue. Modano ni Azam na Chelsea

    ReplyDelete
  3. Tunahitaji kuwa na Viongozi wenye maono na Watendaji mahiri, weledi na wabunifu wa kufuta vyazo vya mapato, ikiwa ni pampja na kushawishi wadhamini kwenye Klabu ya Yanga. Udhamini siyo lazima uwe wa wa fedha nyingi kwa mdhamini mmoja. Ukipata wadhamini wengi hata ama ni kwa kiwango kidogo ukichanaganya na mapato mengine Klabu inakwenda. Tujipange kupata vingozi wenye maono waifikishe mahali Yanga.

    ReplyDelete
  4. Bro Saleh mpira was Sasa unahitaji watu wenye nguvu na kupenda mpira Kama Manji na Mo..angalia ulaya timu zote zinazofanikiwa Ni zile zilizo chini ya matajiri..ksbb Wana uwezo wa kusema..hizi timu ziweke katiba ambayo itampa nafasi mdhamini au mfadhili kuwa na sauti kuliko kuwaacha watu Kama akina akilimali wanapiga kelele wkt hakuna chochote anachochangia..mpira unahitaji matajiri..bila matajiri hakuna maendeleo..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic